Waziri Mkuu Majaliwa Avutiwa Na Mchango Wa NBC Kuchochea Kasi Ya Kilimo, Biashara Na Michezo

  

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameonyesha kuvutiwa na mchango unaoendelea kutolewa na benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika kukuza sekta mbalimbali nchini ikiwemo kilimo, biashara na michezo kupitia huduma na ufadhili wa benki hiyo kwenye maeneo hayo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kulia) akizungumza na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja wa NBC tawi la Lindi Bw. Iovin Mapunda (Kushoto) na Meneja Mahusiano wa beniki hiyo Bi Brendansia Kileo (Katikati) wakati alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili



Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye viunga vya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa saba wa mwaka wa Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Mkoani Lindi. Benki ya NBC ni moja ya wadhamini muhimu wa Mkutano huo wa siku mbili.

Akiwa kwenye banda hilo Waziri Mkuu alipata wasaa wa kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo katika sekta mbalimbali ambapo alionyesha kuvutiwa na huduma ya NBC Shambani inayotolewa na benki hiyo mahususi kwa wakulima wakiwemo wakulima wa zao la korosho.

Waziri Mkuu Majaliwa pia aliipongeza benki hiyo kwa mchango wake kwenye sekta ya michezo hususani udhamini wake kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara yaani NBC Premiere League, Ligi ya Vijana pamoja na NBC Championship.

 

Comments

Popular Posts

Wananchi Makutupora wafunguka changamoto ya Maji, Umeme na Shule kwa Mkuu wa Mkoa

Waziri Mchengerwa apongeza usimamizi wa miradi jijini Dodoma

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma