JIJI LA DODOMA KUPELEKA MIL 50 ZAHANATI YA KIKUYU

Na. Dennis Gondwe, KIKUYU KASKAZINI SERIKALI kupeleka shilingi milioni 50 kukamilisha jengo la wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kikuyu iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kuwafikishia huduma za afya wananchi. Mbunge Anthony Mavunde Kauli hiyo ilitolewa Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi wa Kata ya Kikuyu Kaskazini waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi wa mazingira na upandaji miti kuzunguka Zahanati ya Kikuyu. Mavunde alisema “Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma jengo unaloliona kushoto kwako ni jitihada zangu mimi na diwani wa hapa. Habari njema ni kwamba kabla ya Jumatano wiki ijayo tunaingiza shilingi milioni 50 ambazo zitakwenda kukamilisha jengo hilo. Na nategemea mwezi Oktoba mwaka huu kina mama wataanza kuhudumiwa katika wodi ya wazazi”. Akiongelea historia ya jengo hilo, alisema kuwa mwaka 2020 aliwaahidi wananchi wa kata hiyo kujengewa wodi ya wazazi. “Nilikuja hapa nikiwa na Diwani Mwansasu nikakut...