Mradi wa ukamilishaji Bweni Mbalawala Sekondari
Na. Nancy Kivuyo, MBALAWALA
Kamati ya Siasa
ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma imefanya ziara katika Shule ya
Sekondari Mbalawala kwa dhumuni la kukagua mradi wa ukamilishaji bweni ya wanafunzi
kama moja ya miradi inayopaswa kukamilika na kutumika na wanafunzi wanaotoka
maeneo ya mbali.
Akisoma taarifa
ya mradi wa ukamilishaji wa bweni la wasichana Shule ya Sekondari Mbalawala,
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Fredrick
Mwakisambwe alisema kuwa mradi ulianza kutekelezwa tarehe 14 Mei, 2009 chini ya
usimamizi wa ofisi ya kata hadi hatua na upigaji plasta.
“Ilipofika mwaka 2017 shule ilipokea kiasi cha
shilingi 20,000,000 kutoka mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili shughuli za
ukamilishaji wa kuondoa paa la zamani, kuongeza kozi moja ya tofali, kuweka dari (gypsum board) na kuweka mifumo ya umeme. Kujenga chumba cha matroni, kuskimu na kupaka rangi nje na ndani, kuchimba shimo la choo kwa ajili ya
matundu manne na kujenga
boma la choo hadi kufikia hatua ya lenta. Mwaka 2023 Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilitoa kiasi shilingi
10,000,000 kwa ajili ya kazi zifuatazo za kukamilisha ujenzi wa choo chenye matundu manne na mifumo yake na kuweka mfumo wa umeme katika bweni na
choo” alisema Mwl. Mwakisambwe.
Jengo
la bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mbalawala lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 44 na matroni mmoja na ilianzishwa mwaka 2008 ikiwa na jumla ya wanafunzi
45 ambapo wavulana walikuwa 27 na wasichana walikuwa 18, kwa sasa
shule ina jumla
ya wanafunzi 557, kati
yao wavulana 251 na wasichana 306.
MWISHO
Comments
Post a Comment