Halmashauri ya Jiji la Dodoma yatoa Kongole kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na. Faraja Mbise, NZUGUNI
Halmashauri
ya Jiji la Dodoma inaendelea kutoa shukrani kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa kutenga fedha kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya sekta ya afya kwa
kipindi chote cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita inayopelekea huduma
bora kwa wananchi.
Hayo
yalizemwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Sebastian Pima wakati
akiwasilisha taarifa fupi ya Zahanati ya Mahomanyika kwa Kamati ya Siasa ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma iliyofanya ziara ya kutembelea zahanati
hiyo.
Dkt.
Pima alisema “tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Rais, Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili maboresho ya
miundombinu ya sekta ya afya”.
Akizungumza
kuhusu historia ya zahanati hiyo, alisema kuwa mwaka ambao zahanati hiyo
imejengwa na jumla ya watumishi waliopo wanaowahudumia wananchi wa Mtaa wa
Mahomanyika. “Zahanati ya Mahomanyika ilianzishwa mwaka 1992 na inapatikana
katika Kata ya Nzuguni. Zahanati hii ina jumla ya majengo mawili yambayo ni jengo
la wagonjwa wa nje (OPD) na nyumba ya watumishi. Pia ina jumla ya watumishi
watatu ambao ni mganga mmoja na wauguzi wawili, tuna mahitaji na watumishi 15.
Kwahiyo, upungufu ni watumishi 12, alisema Dkt. Pima.
Halmashauri
ya Jiji la Dodoma, imetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026 kwa ajili ya
kuanzisha ujenzi wa jengo jipya lenye muunganiko na jengo la wazazi kwa lengo
la kusogeza huduma bora za afya karibu na wananchi.
Habari
hii imehaririwa na Dennis Gondwe
MWISHO
Comments
Post a Comment