Mradi wa ujenzi Bweni Nala Sekondari unavutia
Na. Nancy Kivuyo, NALA
HALMASHAURI ya
Jiji la Dodoma yatoa shilingi 25,000,000 kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa
bweni la Shule ya Sekondari Nala kwa lengo la kuwaondolea wanafunzi kero ya kutembea
umbali mrefu kwenda shule na kuongeza ufaulu.
Kauli hiyo
ilitolewa na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl.
Fredrick Mwakisambwe alipokuwa akisoma taarifa ya umaliziaji wa bweni, vyoo na
utengenezaji wa vitanda katika Shule ya Sekondari Nala kwa Kamati ya Siasa ya
Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma.
Mwl.
Mwakisambwe alisema “shule
hii ilianza rasmi tarehe 05 Aprili, 2005 ikiwa na wanafunzi 71. Idadi ya wanafunzi iliendelea
kuongezeka mwaka hadi mwaka na shule kukumbwa na changamoto mbalimbali, mojawapo ikiwa ni wanafunzi wengi
kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani. Hata hivyo, changamoto hiyo ilikuwa kubwa zaidi kwa wanafunzi wa
kike na hivyo,
uongozi wa shule pamoja na bodi
waliomba kujengewa mabweni kwaajili ya wanafunzi wa kike kwa lengo la
kuwaepusha na changamoto ya kukatisha masomo lakini pia kupandisha ufaulu wao
na shule kwa ujumla”.
Alisema kuwa mwishoni
mwa mwaka 2023 shule hiyo ilipokea fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri
ya Jiji la Dodoma kiasi
cha shilingi 25,000,000 kwa awamu mbili kwaajili ya umaliziaji wa bweni moja lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 48,
vyoo matundu manne na utengenezaji wa vitanda 25 ambavyo ni ‘double’ deka za chuma.
“Fedha
hiyo iliingizwa katika akaunti ya shule tarehe 23 Agosti, 2023 kiasi cha shilingi 15,000,000 na
tarehe 20 Septemba, 2023
kiasi cha shilingi 10,000,000.
Katika kutekeleza na kusimamia mradi huu, mfumo wa ‘force account’ ulitumika kufanya malipo ya wazabuni.
Pia, mkuu wa shule aliunda kamati tatu, ambazo ni kamati ya ujenzi, kamati ya
manunuzi na kamati ya mapokezi na ukaguzi. Aidha, utengenezaji wa vitanda 25 ulifanyika
na kugharimu jumla ya shilingi 5,000,000. Kazi hizi zote zilifanyika na
kukamilika kwa gharama ya fedha ya shilingi 21,458,500 ambapo malipo ya
wazabuni yalikuwa shilingi 18,008,500, malipo ya fundi shilingi 3,090,000 na
gharama za Maji
shilingi
360,000.
Aidha,
kiasi cha shilingi 3,541,500 kilibaki kama salio baada ya kukamilika kwa kazi
hizo. Kutokana
na changamoto kubwa ya Maji
hapa shuleni, kamati iliamua kutumia kiasi hiki tajwa kuchimba na kujenga karo
kubwa lenye ujazo wa lita elfu 25 kwaajili ya kuhifadhia maji, ununuzi wa ‘simtank’ moja la lita 5000 na kufunga gata za
kuvunia maji ya mvua” alisema Mwl. Mwakisambwe.
MWISHO
Comments
Post a Comment