Wafanyabiashara wanufaika na ufunguzi wa Nanenane na uzinduzi wa SGR
Na. Rahma Abdallah, NANENANE NA KIKUYU KUISNI
Wafanyabiashara
wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamenufaika kutokana na ufunguzi wa maonesho
ya siku ya Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini
Dodoma pamoja na ufunguzi wa treni ya kisasa ya mwendo kasi inayotumia umeme
(SGR), ufunguzi huo uliofanyika Kata ya Kikuyu Kusini jijini Dodoma.
Hayo yamezungumzwa na wafanyabiashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma mapema jana katika ufunguzi wa maonesho ya Nanenane pamoja ufunguzi wa Treni ya kisasa inayotumia umeme (SGR).
“Nashukuru
Mungu mimi nikiwa kama mfanyabiashara wa chakula nimenufaika sana kwa sababu
watu ni mengi sana hatuna budi kumenya viazi vingi ili wateja wetu wanapokuja
kukuta kila kitu kiko vizuri pia kupitia ufunguzi huu sisi kama wafanyabiashara
tumepata fursa kwasababu kabla ya uzinduzi huu biashara haikuwa nzuri kabisa
kwa sababu ya ukosefu wa watu (wateja) lakini kwa kupitia uzinduzi huu
tumechangamkia na kufanya biashara’’ alisema mfanyabiashara Emmanuel Edward.
Nae,
mfanyabiashara wa chombo cha moto (dereva wa bajaji) anaefahamika kwa jina la Noel
Yonah alisema “siku ya leo ni siku nzuri sana hasa kwetu sisi wafanyabiashara
wa vyombo vya moto kwasababu watu ni wengi sana inafikiwa wakati mpaka mimi
mwenyewe kama mfanyabiashara nachoka kubeba au kupakia wateja. Yaani wateja
wananifata lakini mimi nawaambia mimi siendi kwahiyo, leo tumenufaika sana
tunatamani kila siku biashara iwe kama ya leo’’ alisema Yonah.
Kwa
upande wa mkazi wa Dodoma, Mariam Alex alisema kuwa biashara ni nzuri. “Leo ni
siku ya pesa kama unavyo ona watu ni wengi tena wananchi wa hapa hapa Tanzania.
Mimi nikiwa kama mfanyabiashara ninae uza hizi bendera ndogo za Taifa letu la
Tanzania nimepata pesa nyingi kwasababu kila mtu ananunua bendera ili aonekane
ni mwananchi halali wa Tanzania. Kwahiyo, biashara yangu imeenda vizuri kwasababu
watanzania wenzangu wameniunga mkono namshukuru Mungu, lakini pia nisiwe mchoyo
wa fadhila kuwashukuru na watanzania wenzangu’’ alisema Alex.
Aliongeza
kwa kusema kuwa uzinduzi na ufunguzi ni chanzo cha fursa. Sisi tukiwa kama
wananchi kwasababu, unaweza kubuni na kuanza biashara yako kidogo kidogo na
mwisho kuwa mfanyabiashara mkubwa. “Kwahiyo, sisi kama wananchi hasa vijana
tuache tabia ya uvivu na tujaribu kujishughulisha ili tuweze kukidhi mahitaji
yetu” alisema Alex.
Habari
hii imehaririwa na Fadiga James
MWISHO
Comments
Post a Comment