PM azindua Pikipiki za miguu mitatu kuwawezesha vijana
Na. Flora Nadoo, NANENANE
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa amezindua zoezi la
usambazaji wa pikipiki za miguu mitatu 100 kwa ajili ya vijana katika
viwanja vya Nanenane
jijini Dodoma.
Alisema kuwa pikipiki hizo zitatolewa kwa mkopo nafuu sana
na marejesho hayatakuwa na riba yoyote. “Pikipiki hizi zinamashine ya kusagia
kahawa, sehemu za kukaa watu kwa ajili ya kusambaza kahawa” alisema Waziri Bashe.
Alisema kuwa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO wanatengeneza tera
la miguu mitatu. “Ndani yake zitakuwa na friji dogo, brenda na sehemu za kuonesha mazao. Mtu ataweza akaihamisha au akakaa sehemu
moja ya kudumu. Pia tela hizo
zitakuwa na ‘solar
panel’ kwa
ajili ya kuifanya kazi hiyo. Tunaanza
kugawa kwa ajili ya viwanda”
alisema Waziri Bashe.
Aidha, serikali ilitoa rai kwa vijana wajitokeze kwa wingi kuchukua
pikipiki hizo kwasababu ni chachu ya maendeleo katika jamii na taifa kiujumla. Kupitia
pikipiki hizo zitawasaidia kujikwamua kimaendeleo kutoka hali ya chini kimaisha
hali hali ya juu. Kwa sababu kutokana na teknolojia waliyoitumia kutengeneza
pikipiki hizi ni ya kisasa zaidi hivyo basi, hata kahawa itakayotengenezwa
itakuwa ya kisasa zaidi na utapendwa na watu wengi sana.
Habari hii imehaririwa na Moureen JohN
MWISHO
Comments
Post a Comment