Viongozi wamshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kukuza sekta za Mifugo na Uvuvi

Na. Flora Nadoo, NANENANE

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ameendelea kuzipa kipaumbele sekta za mifugo na uvuvi ili zichangie katika uchumi wa taifa.

 

 

Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan (picha na maktaba)

Shukrani hizo alizitoa wakati akitoa salamu za Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika uzinduzi wa maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni Dodoma.

Mnyeti alisema "Mheshimiwa Rais ameongeza bajeti ya wizara yangu yangu kutoka shilingi bilioni 295.9 mwaka 2023/2024 hadi shilingi bilioni 460.3 kwa mwaka 2024/2025 sawa na nyongeza ya 50.5%. Fedha hizi zitatumika katika kuimarisha sekta ya mifugo na uvuvi na kuongeza mchango wake katika pato la Taifa.

Pia Waziri wa Kilimo Mh.Husein Bashe alianza kwa kumshukuru mgeni rasmi Waziri mkuu Mh.Kasim Majaliwa Kasim kwa kutenga muda wake na kuifanya kazi hiyo.Awashukuru kwa mchango wao mkubwa sana kwenye kilimo.

Hivyo basi, Husein Bashe alimshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 294.97 mwaka 2021/2022 hadi kufikia bajeti iliyopitishwa tarehe 7/6/2024 shilingi trilioni 1.2. Fedha hizo zilizoongezeka zitatumika kwenye kilimo. Pia aliishukuru serikali kutenga fedha kwenye kilimo cha umwagiliaji.

 

Kutokana na mchango wa serikali kwenye kilimo, imepelekea uzalishaji mkubwa sana wa mazao. Aidha, mchango huo umewezesha kufanikisha kupeleka mahindi nchini Zambia kama ilivyokuwa imesainiwa. Mahindi hayo ni jumla ya tani 600,000. Pia kwa mara ya kwanza NFRA imeuza mahindi kwa dola ambayo ni historia ya nchi yetu. NFRA imefungua vituo vya kununua mahindi. Vivyo hivyo, serikali inatoa ruzuku kwenye pembejeo na kwenye bei ya kununua mazao, ili kuwasaidia wakulima na kuwawekea mazingira bora, aliongeza.

 

Alimalizia kwa kusema kuwa serikari yaahidi kwamba hakuna mkulima yeyote wa mahindi ambaye atakosa sehemu ya kuuza mahindi yake. Serikali itanunua mahindi yote yaliyo mikononi mwa wakulima.

 

Habari hii imehaririwa na Emmanuel Lucas kwa kushirikiana na Janeth Gerald

Comments

Popular Posts

Wananchi Makutupora wafunguka changamoto ya Maji, Umeme na Shule kwa Mkuu wa Mkoa

Waziri Mchengerwa apongeza usimamizi wa miradi jijini Dodoma

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma