Serikali kuboresha viwanja vya maonesho ya Nanenane
Na. Moureen John, NANENANE
Waziri
wa Kilimo, Hussein Bashe amesema serikali itaendelea kufanya maboresho katika
viwanja vya maonesho ya Nanenane ikiwa ni mkakati wa kuchangia ukuaji wa uchumi
nchini.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe
Kauli
hiyo aliitoa wakati wa uzinduzi maonesho ya kimataifa ya Nanenane kanda ya kati
katika uwanja wa Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.
Waziri
Bashe alisema “Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo mwaka jana jijini
Mbeya kwamba serikali ianze kufanya mabadiliko ya ujenzi kwa viwanja vya maonesho
ya Nanenane. Kiwanja cha kwanza ni Nzuguni, Dodoma na Mwakangale, Mbeya katika
hali ya kawaida tungesema tumehairisha shughuli za Nanenane mpaka tumalize hali
ya ujenzi lakini tukasema Nanenane itaendelea na ujenzi utaendelea kwa wakati
mmoja. Ujenzi umeanza wa uwanja huu na ujenzi huo utakuwa ni wa awamu tatu
mpaka utakapokamilika na awamu ya kwanza ndio imeanza na ilikuwa shughuli ya
kuondoa watu waliokuwa wamevamia eneo hili tunawahukuru sana wao wenyewe kwa
hiari yao walikubali kuondoka kwasababu wanaamini eneo hili ni mali ya serikali”,
alisema Waziri Bashe.
“Serikali
imeanza na ujenzi wa uzio, uwanja huu utakuwa na maeneo ya vipando, uwanja huu
utakuwa na onesho la mifugo, uwanja huu utakuwa na maonesho ya shughuli za
uzalishaji mwaka mzima. Lakini ndani ya uwanja huu kutakuwa na eneo la ‘conference
facility’ na mikutano. Vilevile, kutakuwa na eneo la ‘incubation centre’ kwa
ajili ya vijana wanaofanya teknolojia na hivi sasa shughuli za ujenzi zimeanza
mpaka awamu zote zitakapokamilika. Serikali itatumia zaidi ya shilingi bilioni
40 kukamilisha miundombinu yote ya uwanja wa Nanenane Nzuguni Dodoma”, alisema Waziri
Bashe.
Aidha,
alimtaarifu Waziri Mkuu wa Tanzania aliyekuwa mgeni rasmi kuwa baada ya
kukamilisha viwanja vya Nzuguni na Mwakangale wataenda hatua ya pili ambayo
itahusisha viwanja vya Morogoro, Arusha, Lindi na Tabora.
Habari
hii imehaririwa na Emmanuel Lucas kwa kushirikiana na Fadiga James
Comments
Post a Comment