DC Shekimweri awakaribisha wananchi kushiriki maonesho ya Nanenane
Na. Tutindaga Nkwindi, DODOMA
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maboresho ya
miundombinu katika viwanja vya maonesho ya Siku ya Wakulima Duniani.
Hayo
aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuwakaribisha
wananchi wote wa Jiji la Dododma na vionga vyake katika maonesho ya Siku ya Wakulima
Duniani yanayohusu tasnia ya uvuvi, kilimo na mifugo yatakayofanyika katika viwanja
vya Nanenane vilivyopo Kata ya Nzuguni, jijini Dodoma.
Alisema
kuwa kwa maonesho ya wakulima duniani kwa mwaka 2025 katika Jiji la Dodoma
yamekuwa na mabadiliko ya hali ya juu. “Kupitia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alitaka mahema yajengwe ya
kisasa na ya kudumu. Hivyo, maagizo hayo tumetekeza kwa kiasi kikubwa. Pia kwa
upande wa barabara tumeweka miundombinu mizuri ya barabara ili kuepusha vumbi.
Hivyo, kwa wale watakaokuja katika viwanja vya maonesho hawatapata vumbi kwa
kuwa miundombinu imeboreshwa” alisema Alhaj Shekimweri.
Pia
aliongeza kwa kusema kuwa maonesho hayo yatakuwa ya kimataifa, kutakuwa na nchi
nane kutoka ukanda wa Afrika zitakazohudhuria na kufanya maonesho katika Jiji la
Dodoma. “Kumekuwa na muamko mkubwa hususani katika taasisi na wadau wa kilimo,
mifugo na uvuvi ambapo wadau wa kilimo zaidi ya 640 wamejisajili kuhudhuria.
Hivyo, kwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa yamefana sana kutokana na ongezeko
kubwa wadau watakaohudhuria kutoka nchi mbalimbali” alisema Alhaj Shekimweri.
Aidha,
mkuu huyo wa Wilaya ya Dodoma aliwakaribisha wananchi wote wanaohitaji
kujifunza mambo mbalimbali kuhudhuria katika maonesho hayo kwasababu ni bure,
yatakayoanza tarehe 01.08.2025 na kufunguliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Phillip
Mpango na kufungwa tarehe 08.08.2025 na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Comments
Post a Comment