Kata ya Ipala ipo mstari wa mbele katika Michezo
Na. Nancy Kivuyo, IPALA Hamasa ya serikali katika michezo nchini ni kichocheo cha wananchi wa Kata ya Ipala kupenda kushiriki michezo ya aina mbalimbali kwa ajili ya kujenga na kuboresha afya zao ili waweze kushiriki katika shughuli za maendeleo. Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Ipala, George Magawa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya michezo katika Kata ya Ipala walipotembelea kata hiyo. Diwani Magawa alisema kuwa serikali imekuwa inafanya hamasa kubwa katika michezo hali iliyopelekea kata yao kuwa na mwamko mkubwa katika kushiriki mashindano mbalimbali yanayoandaliwa katani hapo. āKwakweli, mambo ya michezo tunaenda nayo vizuri, kila mwaka tunafanya mashindano yanayoitwa āMagawa Cupā ambayo diwani ndiye mimi na kwa kushirikiana na mheshimiwa mbunge tuna āMavunde Cupā, tunaandaa mashindano hayo ili kuwasogeza wananchi karibu zaidi na michezo. Wakati mwingine tunaunganisha michezo na kampeni za kijamii za serika...