Mbunge Mavunde akabidhi Kompyuta kwa Kata 41 za Jiji la Dodoma

Na. Nancy Kivuyo, VIWANDANI

Watendaji wa Kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma wapokea Kompyuta na Printa kwa ajili ya kurahisisha na kuboresha utendaji kazi wenye ufanisi za kuwahudumia wananchi.





Vifaa hivyo, viligawiwa katika hafla ya Ugawaji Kompyuta na Printa kwa Shule za Sekondari za Serikali na Watendaji wa Kata jijini Dodoma, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Viwandani.

 Akizungumza wakati wa ugawaji kompyuta hizo, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, alisema kuwa anawapa kompyuta maafisa watendaji wa kata zote 41 kwaajili ya kuwasaidia kufanya kazi zao kidigitali zaidi. “Kompyuta na printa hizi natumaini zitachochea utendaji kazi ulio mzuri. Tuipongeze serikali chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu kwenye sekta ya elimu jijini Dodoma ambapo kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa shilingi bilioni 16” alisema Mavunde.

Nae, Afisa Mtendaji wa Kata ya Hazina, Tunu Mahmoud, alisema kuwa ameguswa na tukio la kipekee la mbunge kuwapa kompyuta za kisasa kwa kwaajili ya utendaji kazi unaoendana na ukuaji wa teknolojia. “Mimi kama mkazi wa Dodoma, suala la elimu lilikuwa nyuma lakini kwa mbunge wetu na waziri, ameona kipaumbele chake ni elimu. Hivyo, nimefarijika na nafurahi sana kwasababu tunaona mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu kwa mchango wake” alisema Mahmoud.





MWISHO

Comments

Popular Posts

Bilioni 9.1 yanufaisha vikundi kwa Mwaka 2020-2023

Mkataba ujenzi Uwanja wa Mpira wa Miguu wasainiwa Dodoma