Dkt. Sagamiko amshukuru Rais Dkt. Samia, Jiji la Dodoma kuwa la mfano
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko,
amshukuru Rais, Dkt. Samia kwa kulifanya jiji hilo kuwa la mfano nchini na
kuahidi utoaji wa huduma bora kwa wananchi alipotembelea banda hilo kwenye
maonesho ya shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Aliyasema hayo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipotembelea banda la Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center kabla ya ufunguzi wa Mkutanao wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).
“Mheshimiwa Rais, Halmashauri ya Jiji la Dodoma ndiyo halmashauri pekee yenye muundo wa kipekee katika halmashauri zote 184 zilizopo Tanzania. Moja ya upekee huo ni Divisheni ya Uendelezaji Makao Makuu. Baada ya Dodoma kuwa makao makuu mwaka 1976 iliweza kuandaliwa Mpango Kabambe wa kuuendeleza Mji wa Dodoma ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Msalato pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)” alisema Dkt. Sagamiko.
Aliongeza kuwa miongoni mwa mipango mingine iliyowekwa ilikuwa ni kutengwa maeneo mengine kwaajili ya makao makuu ya serikali. Baada ya nguvu kazi kuongezeka mwaka 2010 mpango wa kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Mtumba ulifanyika. Pia utekelezaji wa miradi mingine kama ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ulifanyika.
“Mheshimiwa Rais, ulipofika mwaka 2019 ambapo serikali baada ya kuhamia Dodoma, ilifanyika. Pia maboresho kwenye Mpango Kabambe wa makao makuu ya nchi ambapo Dodoma Jiji ndio tupo, na miongoni mwa mambo ambayo tunakushuru ni kwamba ile mikakati na mipango iliyowekwa ikiwemo ujenzi wa ‘outer ring road’, ‘middle ring road’ ambayo bado inaendelea na ‘inner ring road’ ambayo inaendelea ipo kwenye Mpango Kabambe wa Jiji” alisema Dkt. Sagamiko.
Aliendelea kumueleza Rais kuwa, katika muda mfupi wa mwaka 2019-2024 na 2024-2039 ipo mipango iliyokuwa imepangwa kutekelezwa kuanzia 2025 lakini kwenye Mpango Kabambe chini ya serikali imeshatekelezwa kati ya 2019-2024.
“Sisi Jiji la Dodoma ni miongoni mwa watekelezaji ikiwemo ujenzi wa hoteli, shule, vituo vya afya na hospitali. Mheshimiwa Rais, katika mpango huu kabambe wa 2019 eneo hili hapa linaonesha eneo hili (alionesha kwenye ramani) ni Bwawa la Hombolo na mpango huu umeelekeza eneo hili kuwa eneo mahsusi kwaajili ya uwekezaji. Mheshimiwa Rais Jiji la Dodoma katika picha hii unayoiona imekua na Mpango Kabambe ambao umeshaanza kufanya kazi, tunahitaji kuwa na mji wa mfano ‘Thematic satellite City’. Mji huu utaanzia eneo lile la Mtumba, ‘Adjacent’ na mji wa serikali inaenda moja kwa moja mpaka eneo la Hombolo. Katika mkoa wetu wa Dodoma, eneo la Hombolo ndio pekee lina bwawa ambalo halikauki maji kwa mwaka mzima. Kwahiyo, tunataka kutumia eneo hili kuwa mji wa kipekee kabisa wa mfano ili tuwe na mji mmoja unaotokea katika eneo letu” alimalizia Dkt. Sagamiko.
MWISHO
Comments
Post a Comment