Posts
Showing posts from March, 2026
Wanawake watakiwa kulipa kodi na kukuza uchumi katika Jiji la Dodoma
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Wanawake wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, hususan wafanyabiashara na wajasiriamali, wametakiwa kuendelea kulipa kodi na tozo kwa wakati ili kuchangia maendeleo ya jiji pamoja na kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla. Wito huo ulitolewa na Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Zuzu, Pilly Hassan, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 8 Machi, 2026. Alisema kuwa ulipaji wa kodi ni moja ya njia muhimu inayosaidia serikali kupata mapato ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuboresha miundombinu ya masoko, barabara na huduma nyingine muhimu kwa wananchi. “Wanawake wengi wa Jiji la Dodoma tunajishughulisha na shughuli za biashara na ujasiriamali. Hivyo, tunapaswa kuwa mfano mzuri kwa kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu wa kulipa kodi na tozo za serikali kwa hiari na kwa wakati. Kupitia kodi hii itaweza kutusaidia mambo mbalimbali na ya muhimu kama vile kujeng...
Mstahiki Meya Chaula ashauri Baraza kutumia mkakati wa hoja kwa hoja
- Get link
- X
- Other Apps
By Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Na. Mwandishi Wetu, DODOMA Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Alimwoni Chaula ameshauri Baraza la Madiwani kujenga utaratibu wa kuwasilisha hoja moja na kuiazimia hadi itakapokamilika ndio hoja nyingine ifanyiwe kazi. Aliyazungumza hayo kwa msisitizo katika mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri jijini Dodoma. Alisema kuwa mkakati huo wa hoja moja ‘Focus Strategy’ ndiyo njia pekee ya kuleta maendeleo yanayoonekana na yenye tija kwa wananchi wanaowaongoza. "Ili tuwe na ufanisi, niwaombe kwa unyenyekevu mkubwa sana tuchague jambo moja na kuliazimia hadi mwisho. Kwa mfano, kama baraza linaona kipaumbele ni ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule zote za msingi katika jiji letu, basi nguvu, fedha, na usimamizi wetu wote uelekezwe hapo. Tukimaliza na kujiridhisha kuwa kila shule ina vyoo bora, ndipo tunahamia hoja nyingine ya msingi na kuendelea na mtiririko huo" alisema Chaula. Alimalizia kwa kutoa rai kuwa umoja na maamu...