RC Dodoma apongeza wafugaji kwa ushiriki wa Paredi ya Mifugo
Na. Veronica John, DODOMA
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule awapongeza wafugaji kwa kujitokeza kwa
wingi katika shindano la Paredi ya Mifugo Kitaifa 2025 ambalo hufanyika kila mwaka
kuanzia tarehe 1-8 Agosti.
Akizungumza na wafugaji, Senyamule alisema kuwa ameshuhudia mabadiliko na maboresho makubwa katika shughuli za mifugo ambapo hapo awali ilifanyika kikanda na sasa yameenda kimataifa.
Alisema
kuwa mashindano hayo kufanyika sehemu nyingi duniani yakiwa na lengo la
kutambua mchango na juhudi za wafugaji katika kuchangia maendeleo ya taifa na
ya mtu mmoja mmoja. “Maonesho haya huongeza
ari kwa wananchi katika kuinua hadhi ya uzalishaji na tija kwa kutumia
teknolojia mpya zilizoboreshwa katika shughuli za ufugaji ili kukidhi mahitaji
ya soko. Na nimearifiwa kuwa maonesho na mashindano haya yaliasisiwa na Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania mwaka 2010 katika siku ya kilele cha sherehe za maonesho ya Nanenane
Dodoma” alisema Senyamule.
Alimalizia
kwa kusema kuwa idadi ya mifugo imeongezeka kwa kiwango cha kuridhisha. “Katika
juhudi hizo, tumeshuhudia kuongezeka kwa idadi ya mifugo nchini kwa kipindi cha
mwaka 2023/2024 mpaka mwaka 2025 idadi ya mifugo imeongezeka. Kwa maana hiyo, wizara
imeweka vipaumbele katika kuimarisha upatikanaji wa maji, malisho, vyakula vya
mifugo na elimu ya kisasa ya ufugaji.” alimaliza Senyamule.
Nae,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede alikuwa na
machache ya kusema kupitia sekta ya ufugaji kwenye mashindano hayo. “Maonesho
hayo ya Paredi ya Mifugo ni fursa kwa wafugaji kubadilishana taarifa na
teknolojia za ufugaji. Lakini pia kusanyiko hili linawaunganisha wafugaji
pamoja na wataalam wetu ambao wanatoa huduma za mafunzo ya ugani kwenye maeneo
mbalimbali kote nchini. Yote hii ni katika kueneza ujuzi na namna ya kuendeleza
ufugaji katika taifa letu la Tanzania” alisema Dkt. Mhede.
Alimalizia
kwa kuwashukuru wafugaji kwa kujitokeza kwa wingi katika paredi hilo. “Nawashukuru
sana wafugaji kwa kujitokeza kwa wingi na kuleta mifugo yenu ya aina mbalimbali
katika Paredi ya Mifugo hapa ili kuwahamasisha wananchi wengine wanaotarajia kupata
elimu pia kuwa wafugaji bora wa baadae. Hatua hii itaongeza tija ya uzalishaji
kwa kutumia vizuri teknolojia mpya,” alisema Dkt. Mhende.
Imehaririwa na Nancy Kivuyo
Comments
Post a Comment