Zao la Zukini na faida lukuki
Na. Rehema Kiyumbi, DODOMA
Afisa
Kilimo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Nkunde Kimweri amesema kuwa zao la zukini
ni zao lenye vitamini ambalo hutumika kama kiungo cha mboga ili kuleta ladha na
kiafya hutumika kupunguza shinikizo la damu.
Alisema kuwa zao la zukini ni jepesi kupanda na lina matokeo mazuri. ’’Tulitumia mbolea na dawa kutoka Kampuni ya Fomi kuzia na baadae tukatumia Fomi nenepesha ilipoanza kutoa maua. Pia tulitumia dawa ya 40-44 kutoka Kampuni ya Jumbo kudhibiti wadudu na kuhakikisha usalama na ubora wa zao letu, lakini pia tunamshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kutuletea vitu muhimu katika kukuza mazao yetu na hatujapata changamoto yoyote hadi hapa tulipofikia,” alisema Kimweri.
Alimalizia
kwa kuwashauri vijana walio jumbani wakati wakisubiri ajira wajikite katika
kilimo ili kujipatia kipato. ’’Tunawashauri vijana wachukue mikopo inayotolewa
na halmashauri ili wajikite katika kilimo na kujikwamua kiuchumi katika maisha
yao na kama tunavyofahamu kilimo kinamtoa kimaisha kijana kutoka sehemu moja
kwenda sehemu nyingine na hii ni kweli kupitia shuhuda tulizoziona,” alimalizia
Kimweri.
Naye,
Afisa Kilimo Kata ya Zuzu, Michaeli Lukumai alieleza aina ya umwagiliaji
unaotumika na kuhakikisha elimu inatolewa kwa wakulima. ’’Tunatumia umwagiliaji
wa njia ya matone (drip irrigation) na elimu haina mwisho tunaitoa kila siku na
niendelevu ni mojawapo ya jukumu langu kama afisa kilimo kuwaelekeza wakulima
wa kata yangu,” alimalizia Lukumai.
MWISHO
Imehaririwa na Nancy Kivuyo
Comments
Post a Comment