Wananchi Matumbulu kufurahia ujenzi ofisi mpya ya Kata
Na. Nancy Kivuyo, MATUMBULU
SERIKALI
ya awamu ya sita inalenga kuboresha mazingira bora ya kufanyia kazi kwa
wafanyakazi wa serikali ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kujenga
na kuboresha Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Matumbulu, Halmashauri ya Jiji
la Dodoma.
Kauli
hiyo ilitolewa na Afisa Mtendaji Kata ya Matumbulu, Zubery Mbawala alipokuwa
akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa waandishi wa habari
waliofanya ziara ya kutembelea miradi iliyotekelezwa na serikali katika Kata ya
Matumbulu, jijini Dodoma.
Mbawala
alisema kuwa ujenzi wa Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Matumbulu ulianza kwa
michango ya nguvu za wananchi. “Wananchi walijitolea eneo na wakaanza ujenzi
kwa nguvu zao, baadae serikali ndio ikawapokea, kuendeleza ujenzi huo kwa kutoa
kiasi cha shilingi 67,000,000 ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika na
wananchi wanapata huduma bora. Hata sasa ofisi hii inatumika japo ipo katika
hatua za mwisho kukamilika” alisema Mbawala.
Aliongeza kuwa ofisi hiyo kwa miaka minne ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha eneo la utawala bora. Huduma tunazotoa zimeendelea kuistawisha kata yetu hata sasa kuna utulivu, amani na shughuli za maendeleo zinafanywa kwa ufanisi mkubwa sana. Hivyo, tunaishukuru serikali kwa jitihada hizi kubwa za kuhakikisha wananchi wanasogezewa huduma muhimu kwenye maeneo yao” alimalizia Mbawala.
Nae
Diwani wa Kata ya Matumbulu, Emmanuel Chibago alisema kuwa kuanzia mwaka 2020
hadi 2025 serikali imefanya kazi nzuri katika kuwapelekea maendeleo wananchi
yanayochochea ushiriki katika uanzishwaji wa miradi ya maendeleo. “Tunawapongeza
wananchi kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Sio tu ofisi ya
kata wameianzisha wao, miradi mingine mingi ni wao ndio waanzilishi,
tunawapongeza kwa hilo” alisema Chibago.
MWISHO
Comments
Post a Comment