Shekimweri awaita mashabiki wa Dodoma Jiji FC, Ally Hassan Mwinyi
Na. Nancy Kivuyo, DODOMA
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri ameitakia kila la kheri timu ya Dodoma
Jiji FC katika mchezo wao ujao dhidi ya Tabora United FC, utakaopigwa katika dimba
la Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akielezea jambo |
Alizungumza
hayo wakati akitoa salamu katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
“Licha
ya changamoto timu yetu iliyopitia, timu imeweza kufanya vizuri katika michezo
miwili mtawalia. Timu hii ni fahari ya nchi ikiiwakilisha makao makuu ya nchi. Hivyo,
tunawatakia kila la kheri katika mchezo wao dhidi ya Tabora United FC
watakaocheza ijumaa. Tunawasisitiza wadau na wana Dodoma kwenda kuipa nguvu
timu yetu ili matokeo yawe mazuri” alisema Shekimweri.
Naye,
Elice Kitendya alisema “kwakua mimi ni mdau mkubwa wa timu yetu ya Dodoma Jiji,
nina matumaini makubwa na timu yetu, mashabiki tunawahimiza wenye nafasi ya
kwenda Tabora tujumuike pamoja kwenda kuisapoti timu yetu ili wapate morali ya
kutosha. Niseme tu kwamba, ninaamini watafanya vizuri ili kuendeleza ushindi
ambao tumeuanza”.
Timu
ya Dodoma Jiji FC itaondoka kesho kuelekea mkoani Tabora kwaajili ya mechi yao
dhidi ya Tabora United FC, mchezo utakaopigwa katika dimba la Ally Hassan
Mwinyi siku ya Ijumaa majira ya saa nane mchana, katika mechi ya mzunguko wa
kwanza Dodoma Jiji FC iliibuka kidedea kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-0.
Katika michezo mitatu ya mwisho ya ligi Dodoma Jiji FC imekusanya alama saba
kibindoni.
MWISHO
Comments
Post a Comment