Wanafunzi Chamwino wahimizwa kula mboga za majani
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO
WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Chamwino wametakiwa
kula kwa wingi mboga za majani ili kuwa na lishe bora itakayowasaidia kusanya
vizuri katika masomo yao.
![]() |
Afisa Lishe kutoka Kituo cha Afya Makole, Ezeleda Mongo (mwenye tisheti nyeupe) akiwafundisha wanafunzi jinsi ya kusia mbegu |
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Lishe kutoka Kituo cha
Afya Makole, Ezeleda Mongo alipokuwa akiongea na wanafunzi, walimu na wadau wa
lishe katika tukio za kusia mbegu za mboga za majani katika Shule ya Msingi Chamwino.
“Nimefurahi
kujumuika nanyi katika hili zoezi la kuhamasisha mazoezi na zoezi la upandaji
wa mbogamboga. Ninashauri sana jamii itumie mbogamboga na matunda zaidi kwa
ajili ya kuhamasisha afya. Magonjwa yasiyo ambukiza yanaweza kutibika kwa njia
ya chakula hususani mbogamboga na matunda” alisema Mongo.
Aidha,
aliwashauri wanafunzi kuwa wanakula mbogamboga kwa wingi. “Wito wangu hata kwa
watoto wa shule wanapokuwa wanaendelea kukua wale mbogamboga za majani kwa
wingi. Ndio maana leo tumekuja kuonesha upandaji wa mbogamboga ili ziwe
zinapatiokana kwa wingi katika shule zetu. Hii itatusaidia kupata watoto wenye
uelewa mzuri na wenye afya njema” alisema Mongo.
Kwa
upande wake Joseph Malolela kutoka Chama cha Baiskeli Mkoa wa Dodoma alisema
kuwa waliamua kuendesha baiskeli kwa ajili ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza hususani zoezi la uhamasishaji lishe bora. “Wadogo zetu nawaomba
sana mjitahidi kufanya mazoezi ya kuendesha baiskeli yanaimarisha afya.
Mnaniona mimi nilivyo, hii yote ni sababu ya baiskeli, baiskeli inajenga afya
inakuwa safi na inakusaidia kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Baiskeli inasaidia kuimarisha akili na mwili” alisema Malolela.
Zoezi
la kusia mbegu za mboga katika Shule ya Msingi Chamwino lilitanguliwa na mbio
za baiskeli zilizolenga kuhamaisha afya bora dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambuza
na kuchochea masuala ya lishe bora kwa jamii.
MWISHO
Comments
Post a Comment