Mkuu wa Mkoa wa Dodoma atembelea Kijiji cha Mitambo, Nanenane

 




Mkuu wa Mkoa, Rosemary Senyamule Agosti 7, 2025 ametembelea Kijiji cha Mitambo (Mechanisation Village) kilichosheheni teknolojia mbalimbali za kilimo cha umwagiliaji kinachopatikana katika Maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi maarufu kama Nanenane Kitaifa 2025 Kanda ya Kati yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini hapa.

Vilevile, Senyamule akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, wametembelea mabanda kadhaa yakiwemo; Tume ya Ushindani, Chuo cha Biashara na Elimu (CBE), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Madini (STAMICO), VETA, Wizara ya Maendeleo ya Jamii na TBA na kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hizo

Comments

Popular Posts

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ni nyenzo ya utendaji kazi serikalini – Dkt. Biteko

JIJI LA DODOMA KUPELEKA MIL 50 ZAHANATI YA KIKUYU

WENZA WA VIONGOZI WASHAURIWA KUANZISHA BUSTANI ZA NYUMBANI