Na. Mwandishi wetu, MSALATO Wananchi wa Jiji la Dodoma wametakiwa kuendesha biashara saa 24 huku wakihakikisha usafi wa mazingira unafanyika muda wote, ili huduma ziendelee kupatikana bila kuathiri usafi wa maeneo yao. Rai hiyo imetolewa wakati wa Uzinduzi wa Kampeni Endelevu ya Usafi wa Mazingira katika eneo la Mnada wa Msalato, jijini Dodoma, ambapo ilisisitizwa kuwa dhana ya “biashara saa 24” inapaswa kwenda sambamba na “usafi saa 24.” Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alisema kuwa maafisa afya pamoja na watendaji wa kata na mitaa watakuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya biashara ili kuhakikisha usafi unazingatiwa muda wote. “Biashara masaa 24, lakini usafi masaa 24. Maafisa afya, watendaji wa kata na mitaa watakuwa wakipita kufanya ukaguzi, na atakayekaidi maelekezo ya usafi atatozwa faini ya shilingi 50,000 hadi shilingi 300,000,” alisema Alhaj Shekimweri. ...
Na. Mwandishi wetu, NZUGUNI Wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi wametakiwa kuchukua tahadhari mapema dhidi ya mvua za El Nino, ikiwemo kuepuka maeneo yanayoweza kukumbwa na mafuriko na kuhakikisha usalama wa familia zao. Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa bwawa la kuvunia maji ya mvua katika viwanja vya Dkt. John Malecela (Nanenane), Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri alisema kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi wanapaswa kuzingatia tahadhari zinazotolewa na mamlaka. Alisema kuwa wananchi wanaoishi mabondeni, karibu na mito na maeneo yanayoweza kuathiriwa na mafuriko wanapaswa kuwa makini na kuchukua hatua mapema ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa. Aidha, aliwataka wananchi kuhakikisha mifereji na njia za maji hazizibwi kwa taka, akieleza kuwa hali hiyo inaweza kuzuia mtiririko wa maji na kuongeza uwezekano wa kutokea kwa mafuriko katika maeneo ya makazi. Katika ziara hiyo, ...
Na. Amoni Sambulila, MSALATO Wananchi mkoani Dodoma wamehimizwa kufanya usafi wa mazingira kila siku na kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakuwa safi na salama kwa afya na ustawi wa jamii. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi wa Mazingira mkoani Dodoma, uliofanyika katika eneo la Mnada wa Msalato, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyemule alisema kuwa kufanya usafi ni wajibu wa kila mwananchi na si jukumu la taasisi au mamlaka pekee. Aliongeza Kwa kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi, kutunza maeneo yao na kuendelea kuzingatia usafi wa mazingira katika maisha yao ya kila siku. Kwa upande wake, mwananchi wa Msalato, Juma Ally alisema kuwa ushiriki wa jamii ni muhimu katika kuhakikisha kampeni hiyo inakuwa na matokeo chanya na kuleta mabadiliko katika maeneo mbalimbali. Nae, mwananchi wa Msalato, Neema Ramadhani aliwahimiza wananchi kufanya usafi kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku, ikiwemo kutunza maeneo ya makazi na maene...
Comments
Post a Comment