Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Jiji la Dodoma atoa hakikisho ofisi kufunguliwa na kufungwa kwa wakati siku ya mwisho kuchukua na kurudisha fomu
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Halmashauri
ya Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko amewataka viongozi wa vyama 19 vya
siasa kuwahamasisha wananchi kuchukua na kurejesha fomu akiwahakikishia kuwa
ofisi zitafunguliwa na kufungwa kwa muda uliopangwa.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi |
Dkt. Sagamiko alitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi kuwakumbusha wananchi kuwa ni siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa.
“Leo tarehe 1 Novemba, 2024 ni siku ya mwisho ya kuchukua
na kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa. Ofisi
zimefunguliwa mapema zaidi ili saa 2:00 asubuhi kuanza kutoa huduma hadi saa
10:00 jioni. Hakuna ofisi itakayochelewa kufunguliwa wala itakayowahi kufungwa.
Hivyo, viongozi wa vyama vyote 19 niwaombe kuwahimiza wanachama wenu kuchukua
na kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa. Puuzeni
taarifa zozote za kuelezea kuwa ofisi zitakuwa zimefungwa” alisema kwa msisitizo
Dkt. Sagamiko.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt. Frederick Sagamiko |
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina vituo
222, wakati zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za uongozi
lilianza tarehe 26 Oktoba, 2024 na kuendelea hadi leo tarehe 1 Novemba, 2024.
MWISHO
Comments
Post a Comment