Ofisi wazi kuchukua na kurejesha fomu za wagombea nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa
Na. Asteria Frank, DODOMA
Vituo 222 vya Ofisi
za Mitaa ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma zimefunguliwa mapema zaidi leo tarehe
1 Novemba, 2024 kwa lengo la kuweka upana mkubwa kwaajili ya kuchukua na
kurejesha fomu za wagombea nafasi ya uongozi Serikali za Mitaa.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Frederick Sagamiko |
Kauli hiyo ilitolewa
na Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt.
Frederick Sagamiko asubuhi ya leo katika ofisi yake wakati akizungumza na waandishi
wa habari akiuhabarisha umma kuhusu tamati ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji
wa fomu za kugombea uongozi wa serikali za mitaa katika Jiji la Dodoma.
Dkt. Sagamiko
alisema “hakuna ofisi yoyote katika Jiji la Dodoma ambayo itafungwa wakati zoezi
hilo likiendelea. Naomba nitoe rai kwa viongozi wa vyama vya siasa vyote 19
katika Jiji letu la Dodoma kuhakikisha wanatumia siku hii muhimu ambayo ni siku
ya mwisho kuhakikisha wagombea wanaowakilisha vyama vyao wanachukuwa fomu na
kurejesha kwanzia muda wa saa 2:00 asubuhi na mwisho itakuwa ni saa 10:00 jioni,
ofisi zetu zitakuwa wazi kwa masaa nane”.
Zoezi la
kuchukua na kurudisha fomu za kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa
lilianza tarehe 26 Oktoba, 2024 na litakamilika leo tarehe 1 Novemba, 2024 saa
10 jioni.
MWISHO
Comments
Post a Comment