RC aishukuru Serikali kupeleka Nanenane kitaifa Dodoma
Na. Fadiga James, NANENANE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameishukuru
serikali kwa kuamua maonesho ya Nanenane kitaifa kufanyikia Dodoma na kusema ni
fursa kwa wananchi wa mkoa huo kunufaika kiuchumi.
Senyamule alitoa shukrani hizo wakati akitoa
salamu za Mkoa wa Dodoma kwenye ufunguzi wa maonesho ya Nanenane kitaifa yaliyofanyika
Kanda ya Kati uliofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania katika viwanja vya Nanenane,
Nzuguni jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameishukuru serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanikisha sherehe za Nanenane
kufanyika jijini Dodoma na kusema kuwa ni mahali sahihi kwasababu wakulima na
wafugani ni wengi na yatasaidia wananchi kukua kiuchumi.
“Kipekee nishukuru sana kwa dhati kuwa mwaka huu
2024 maonesho ya Nanenane yanafanyika Kanda ya Kati kitaifa katika Mkoa wa Dodoma.
Tunashukuru sana kwasababu ni historia ya muda mrefu kidogo, tulishaanza
kusahau kuandaa hata haya maonesho ya kimataifa, lakini tutoe shukrani nyingi
kwa mheshimiwa Rais, lakini tutoe shukrani nyingi kwa Wizara ya Kilimo na
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa uamuzi huu” alisema Senyamule.
Akitumia ufunguzi huo kuwataka wakazi wa Dodoma
kuchangamkoa fursa ya maonesho hayo kufanyikia Dodoma kukua kiuchumi. Alisema
kuwa ni fursa kwa makundi yote kuchangamka kujifunza teknolojia mpya za kilimo
na ufugaji na kunufaika na wingi wa watu kufanya biashara mbalimbali na kukua
kiuchumi.
MWISHO
Comments
Post a Comment