Rais, Dkt. Samia: SGR siyo ndoto tena
Na. Janeth Gerald, KIKUYU KUSINI
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua treni
ya mwendokasi (Standard Gauge Railway) na kuandika historia baada ya miaka 114
ya Tanzania kujenga reli ndefu na kusema kuwa mradi wa SGR siyo ndoto tena,
bali ni uhalisia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miundombinu
na safari za treni kati ya Dar es salaam na Dodoma kupitia Morogoro alisema
kuwa aliupokea mradi huo kutoka kwa watangulizi wake na kuufikisha hapo.
Alisema kuwa katika miaka mitatu ya uongozi
wa serikali ya awamu ya sita, wamekamilisha ujenzi wa vipande viwili vya Dar es
salaam hadi Morogoro na Morogoro hadi Dodoma.
"Kwa sasa kazi inaendelea katika vipande
vya Makutupora hadi Tabora kilometa 368, Tabora hadi Isaka kilometa 341, na
Isaka hadi Mwanza kilometa 341. Pia serikali inajenga Tabora hadi Kigoma,
kipande chenye urefu wa kilometa 565, ambayo itajumuisha kuingia katika nchi za
Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Nchi zilizoendelea
hazikutaka kuona Tanzania inakamilisha mradi huu wa SGR kwasababu zinafahamu
kuwa mradi huu ukikamilika Tanzania inafuta umasikini. Pia kuna mzigo mkubwa
kati ya nchi ya DRC na nchi nyingine jirani ambao utasaidia Bandari ya Dar es
salaam kuwa na mzigo wa kutosha na kutengeneza faida kubwa" alisema Dkt.
Samia Suluhu Hassan.
Aidha, alilitaka Shirika la Reli nchini
kuendesha treni hiyo kibiashara na kutotegemea ruzuku ya serikali bali kutoa
gawio la mwaka kwa serikali baada ya kutengeneza faida.
MWISHO
Comments
Post a Comment