Rais Samia asisitiza kuendelezwa kwa ubora wa reli ya SGR
Na. Fadiga James, KIKUYU KUSINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirika la Reli nchini (TRC) kuhakikisha ujenzi
wa reli ya SGR unaendelea kufanyika kwa ubora wa hali ya juu.
Agizo hilo alilitoa wakati wa uzinduzi wa stesheni
ya SGR Dodoma iliyopo Kata ya Kikuyu Kusini jijini Dodoma.
Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema kuwa
TRC na menejimenti yake kusimamia ujenzi wa reli ya SGR kwa ubora wa hali ya
juu. Reli ikijengwa vizuri itaweza kudumu kudumu na kunufaisha nchi kwa muda
mrefu, aliongeza.
"Bodi ya wakurugenzi na menejimenti ya
TRC, hakikisheni vipande vya reli hii inayoendelea kujengwa ya SGR,
vinakamilika kwa wakati na ubora uliokubariwa" alisema.
Vilevile, aliiagiza TRC kuhakikisha huduma
zinazotolewa ndani na nje ya treni zinakuwa za ubora ili kuvutia zaidi watalii
wa ndani na nje ya nchi na kuhakikisha usalama wa abiria na mali zao ndani ya
treni hiyo.
MWISHO
Comments
Post a Comment