Wanawake Dodoma watakiwa kujishughulisha
Na. Dennis Gondwe, MSALATO
WANAWAKE
wametakiwa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali ili kuweza kukuza
kipato cha familia na taifa kwa ujumla kutokana na fursa za kazi zilizopo
katika Mkoa wa Dodoma.Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Mwl. Neema Majula akiongea na wanawake waliohudhuria Kliniki Zahanati ya Msalato
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Dodoma, Mwl. Neema Majula alipokuwa akiongea na wanawake katika maadhimisho ya siku ya wanawake Kata ya Msalato yaliyofanyika katika Zahanati ya Msalato katika Kata ya Msalato.
Mwl.
Majula alisema kuwa kila mwanamke katika Mkoa wa Dodoma anatakiwa
kujishughulisha ili kukuza kipato cha familia na taifa. “Ndugu zangu wakati
mwingine ukatili wa kijinsia unatokana na kina mama kutokujishughulisha na
uzalishaji mali katika ngazi ya familia. Hivyo, unyanyasaji unakuwepo kwa
sababu kila kitu unamtegemea baba alete. Nataka nikwambie ukifanya kazi kwa
bidii mfano ukianzisha biashara, ukafuga kuku hata ng’ombe, ukafungua duka au
kigege na chenji hazikutoki hata unyanyasaji katika familia hautakuwepo, baba
atakuheshimu kwa sababu una pesa” alisema Mwl. Majula.

Alisema
kuwa Mkoa wa Dodoma una fursa nyingi za kujiendeleza kiuchumi kutokana na kuwa
na watu wengi waliohamia baada ya kuwa makao makuu. Fursa ya wingi wa watu
ndiyo fursa ya kufanya biashara na kufanya kilimo cha mazao mbalimbali,
aliongeza.
MWISHO
Comments
Post a Comment