Wanasheria waanza mwaka mpya wa Mahakama
Na. Leah Mabalwe, DODOMA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua rasmi
mwaka mpya wa Mahakama 2024 na kuwatakia wanasheria wote kheri ya mwaka mpya wa
mahakama ulioanza Februari 1, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa Mahakama ya Rufaa |
Kauli hiyo aliitoa katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika bustani ya mapumziko Chinangali jijini Dodoma.
“Tunaanza
rasmi mwaka wa Mahakama na tunawakumbusha kuwa na mchango katika utendaji kazi
kwa wadau wote wa Mahakama nchini, na nawakumbusha kufanya kazi kwa kuzingatia
viapo vyenu vya utendaji kazi mlivyo viapa wakati wa kuanza kazi hii” alisema
Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha,
aliongezea kwa kuwapongeza watumishi wote wa Mahakama kwa kufanya kazi nzuri
kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao. “Nawapongeza sana waheshimiwa Mahakimu,
wasajili wa mahakama kuu, majaji wa mahakama za rufaa na watumishi wote wa
mahakama kwa namna ambavyo mnavyoendelea kutekeleza majukumu yenu, nawapongeza
sana,” alisema Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa
upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma ampongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kudumisha mfumo wa utoaji haki jinai. “Jitihada
zako za kuijenga Tanzania ya maendeleo na haki kwa jamii inayozingatia misingi
ya uhuru, haki na undugu na amani, hata hivyo utashi wako umedhihirika pale
ulipounda Tume ya Haki Jinai kuanzisha kwa kampeni ya msaada wa kisheria ni
miongoni mwa jitihada zako za utashi wa kiserikali na kuimarisha mfumo wa
utoaji haki” alisema Prof. Juma.
Maadhimisho
ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka tarehe 1 Februari na kwa mwaka
2024 maadhimisho yalifanyika jijini Dodoma yakiongozwa na kaulimbiu ‘Umuhimu wa
dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa, nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha
Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai’.
MWISHO
Comments
Post a Comment