Wanasheria watakiwa kufuata misingi ya Uadilifu
Na. Arafa Waziri, DODOMA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwataka wanasheria
nchini kufanya kazi kwa kufuata misingi ya uadilifu na kutenda haki.
![]() |
Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongea katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini |
Aliyasema
hayo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika jijini
Dodoma na kuwataka wanasheria wote nchini kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na
kutenda haki kwa wananchi. “Mnalazimika kusimama katika misingi ya dini pamoja
na Katiba ya Tanzania. Mna dhima mbinguni na Duniani kwahiyo, mna wajibu wa
kutenda haki ili kuweka amanikwa wananchi” alisema Dkt. Hassan
Lakini
pia aliwapongeza wanasheria kuendelea kufanya kazi ya kusaidia wananchi kupata
haki na kuwasisitiza kuwa na ushirikiano baina yao ili kubaini mapungufu
yaliyopo na kuchukua hatua kwa pamoja. “Niwapongeze kwa namna mnavyoendelea
kutimiza
majukumu
yenu na hii ni ushahidi tosha kwamba mnafanya kazi kubwa na kwamba Mahakama
inakwenda na mabadiliko kutoka hatua moja kwenda nyingine” alisema Dkt. Hassan.
Pia
alisema kuwa katika kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
serikali imeeendelea kuweka mazingira mazuri kwa kushirikiana na Mahakama ili
kuongeza ufanisi katika kutoa haki kwa wananchi.
“Serikali
kwa upande wetu tunaendelea na mkakati wa namna ya kuteleza Ilani ya CCM kwa
kuongeza wigo mpana katika kutatua sheria lengo likiwa ni kuongeza ufanisi kwa
kuongeza idadi ya watenda kazi wa Mahakama ili kupunguza mrundikano wa kesi”
alisema.
Nae
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma alimshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa katika Mahakama, huku akiahidi kuwa
wataendelea kutoa mchango mkubwa katika kuweka haki na uadilifu. Vilevile,
alitoa wito kwa wadau wa sheria kuendelea kuungana kutoa ushirikiano lengo ni
kuwa na haki katika jamii. “Maboresho ya miundombinu katika Tehama yamesaidia
kupunguza mrundikano wa kesi na tuhaahidi kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa
ufanisi mkubwa na tunaomba wadau wengine wa sheria waendelee kujitokeza na kutoa
ushirikiano ili kuhakikisha utendaji wa Mahakama unakuwa na matokeo kwa jamii”
alisema Prof. Juma.
Siku
ya Sheria nchini ilihitimishwa jijini Dodoma ikiwa na kaulimbiu isemayo ‘Umuhimu
wa dhana ya haki kwa ustawi wa taifa, nafasi ya Mahakama na wadaau katika
kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai’
MWISHO
Comments
Post a Comment