Na. Coletha Charles, MIYUJI Diwani wa Kata ya Miyuji, Beatrice Ngerangera, ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni saba kutekeleza miradi ya maendeleo katika kata yake na kusema kuwa miradi hiyo imebadilisha maisha ya wananchi na kuyafanya kuwa bora zaidi. Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Kata ya Miyuji kwa kipindi cha mwaka 2021-2025 na serikali. Alisema kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa miradi ya Kata ya Miyuji kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi. “Katika kipindi cha miaka minne, kata yetu ya Miyuji imenufaika na miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7. Hii ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari yenye miundombinu kamili kuanzia ‘O-Level’ hadi ‘A-Level’, ikiwa na mabweni na nyumba za walimu. Gharama yake ni shilingi 544,000,000 kutoka serikali kuu kupitia SEQUIP” alisema Diwani Ngerangera. ...
Comments
Post a Comment