Usafi wa Mazingira Kipaumbele Kata ya Chamwino
Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO CLUB ya Mazingira ya Shule ya Sekondari Hijra imeshiriki zoezi la usafi wa mazingira pembezoni mwa barabara inayoelekea katika makaburi ya Hijra urefu wa takribani mita 200 kwa kufyeka majani, kuokota taka ngumu na makopo ili kuweka viunga vya barabara hiyo safi. Akitoa shukrani baada ya zoezi hilo, Afisa Mtendaji Kata ya Chamwino, Lucas Mkelege alisema kuwa uongozi wa Shule ya Sekondari Hijra umeonesha mfano mzuri kupitia Club yake ya Mazingira. “Mtakumbuka kuwa tangu kuanzishwa kwa Club ya Mazingira katika Shule ya Sekondari Hijra mwaka 2023 imekuwa mstari wa mbele katika suala ya usafi wa mazingira. Nakumbuka malengo ya club hiyo pamoja na mambo mengine ni kuwajengea wanafunzi moyo wa uzalendo na kushiriki masuala ya kijamii ikiwemo kudumisha usafi wa mazingira, asanteni sana” alishukuru Mkelege. Kata ya Chamwino imekuwa mstari wa mbele katika masuala ya usafi wa mazingira ikiwa na muitikio mkubwa wa wananchi kushiriki usafi wa pamoja wa mazingira. ...