Shule ya Msingi Chinangali wapewa elimu ya Uzalendo
Na. Leah Mabalwe, CHAMWINO
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Chinangali Kata ya Chamwino wapewa elimu juu ya uzalendo wa nchi
yao.
Hayo
yalijili baada ya Afisa Ushilikishwaji wa Jeshi la Polisi Kata ya Chamwino, A/Insp
Isiaka Shabani kutembelea shule hiyo na kutoa mafunzo ya uzalendo na kusema
kuwa kila wanafunzi ni jukumu lake kuwa mzalendo.
“Kila
mwanafunzi ni jukumu lake kuwa mzalendo na kuachana na matendo mabaya ambayo
yanajikita katika ukatili na badala yake kuwa mzalendo katika Taifa lake kwa
kumtolea mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan” alisema A/Insp. Shabani.
Aidha,
aliongeza kwa kuwataka wanafunzi hao kujua umuhimu wa Bendera ya Taifa maana
yake hususani rangi zinazopatikana katika Bendera ya Taifa ni kielelezo kikubwa
cha Taifa.
Pia
alimalizia kwa kuwasihi wanafunzi hao wa
Shule ya Msingi Chinangali kuwa inapaswa
kuwa mzalendo popote pale watakapo
kuwepo na uzalendo huanzia ndani ya moyo wa mtu na kila Mtanzania ni jukumu
lake kuwa mzalendo.
Nchi
ya Tanzania ni nchi mojawapo kati ya nchi ambazo zinadumisha na kuendeleza
uzalendo katika nchi na kila mtu ni jukumu lake kuipenda na kuidhamini nchi
yake na kuweka maslahi ya taifa lake mbele Neno uzalendo
linamaana kubwa katika nchi yetu na nijukumu
letu sote sisi kama Watanzania kuidhamini
Nchi yetu.
MWISHO
Comments
Post a Comment