Mradi wa Polisi Jamii "FAMILIA YANGU HAINA UHALIFU" wapokelewa vizuri Kata ya Chamwino
SP
Dr. Ezekiel Kyogo, kutoka Makao Makuu ya Polisi, Kamisheni ya Polisi Jamii kwa
kushirikiana na Afisa ushirikishwaji wa Jeshi la Polisi wa Kata ya Chamwino
A/Insp. Isihaka Shabani wameshirikiana kutoa Elimu ya Mradi wa Polisi Jamii
unaoitwa "Familia yangu haina Uhalifu" kwa wananchi wa Mtaa wa
Mwaja (eneo la Kidongo chekundu), Kata ya Chamwino.
Wananchi wamefundishwa kuelimishwa kuepukana na uhalifu ngazi ya familia kama ifuatavyo:-
1. Wananchi
wamefundishwa ni changamoto zipi katika ngazi ya familia ambazo hupelekea Mtu
kuingia kwenye uharifu lakini pia waliwakumbusha wazazi wawe mfano kwa
kuonyesha tabia nzuri ili watoto waige mazuri yao.
2. Ni Muhimu sana wazazi wawe marafiki wa watoto ili kujua changamoto zao pamoja na kuwa na kauli nzuri kwa watoto ili wasikate tamaa na kuingia kwenye makundi ya uhalifu.
3. Wazazi wamehimizwa kuwajenga watoto mapema namna ya kujitegemea ili wawe na tabia ya kupenda kufanya kazi.
4. Wazazi wamekumbushwa kuwa na tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wao pamoja na Kukagua miili yao kuona kama wanakumbana na matendo ya ukatili.
Pamoja na hayo, ni
wajibu wa wazazi au walezi kuhakikisha kua watoto wanapata mahitaji yao muhimu
na wanawajibika kwa watoto kwani ni takwa la Sheria namba
21 ya mtoto ya mwaka 2009, hivyo Watoto wakipata malezi bora ndani ya familia
basi jamii haitokua na wahalifu kabisa.
Mwisho, wananchi wa Kata ya Chamwino, wamelishukuru Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu, Kamisheni ya Polisi Jamii kwa Elimu waliyoitoa ili kuzuia uhalifu katika ngazi ya Familia na wamehaidi kuitumia elimu hiyo kila wakati Ili kuhakikisha hakuna matukio ya uhalifu ngazi ya Familia.
*#FamiliaYanguHainaUhalifu*
*#JeshiLaPolisi*
*#KataYaChamwino*
*#TheCityCouncilOfDodoma*
Imetolewa na Ofisi
ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Comments
Post a Comment