KISASA SEC YANUFAIKA NA UWEKEZAJI WA RAIS, DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
SHULE ya Sekondari Kisasa ni mnufaika wa uwekezaji
mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia
Suluhu Hassan katika sekta ya elimu na kuchangia kuongeza kiwango cha ufaulu.
![]() |
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisasa, Mwl. Fredy Nyandoro alipokuwa akisoma taarifa ya shule |
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari
Kisasa, Mwl. Fredy Nyandoro alipokuwa akisoma taarifa ya shule hiyo katika
Mahafali ya 15 ya kidato cha Nne ya shuleni hapo.
Mwl. Nyandoro alisema “ndugu mgeni rasmi, shule yetu
tumekuwa na mafanikio kadhaa tangu kuanzishwa mwaka 2006. Mafanikio hayo ni
kuongeza ufaulu mwaka hadi mwaka, kuongeza idadi ya watahiniwa na idadi ya
vijana wanaojiunga elimu ya juu na vyuo vya kati imeongezeka. Shule imefanikiwa
kuongeza miundombinu mwaka 2019 tulianza kujenga jengo la utawala na
limekamilika. Mwaka 2021 tukapata mradi wa kuongeza madarasa kwa fedha za
Uviko- 19 tulikuwa na madarasa matatu na kufanya madarasa kufikia 23.
Tunaishukuru sana serikali yetu na mama yetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan kwa uwekezaji mkubwa ambao ameufanya katika sekta ya elimu na Shule ya
Sekondari Kisasa ni mnufaika mkubwa wa uwekezaji huo”.
Mafanikio mengine aliyataja kuwa ni kupata vifaa vya
kutosha vya maabara za sayansi mwaka wa fedha 2021/2022. “Mwaka 2023 tumepokea
zaidi ya vitabu 2,000 vya masomo mbalimbali. Shule yetu ina maktaba bora
niongoni mwa shule za sekondari nchini. Maktaba yetu imesheheni vitabu lakini
pia tuna mfumo wa Tehama na pale vijana wetu wanaposoma, wanasoma kwa utulivu
tuna kiyoyozi” alisema Mwl. Nyandoro kwa furaha.
Kwa upande wa mwanafunzi wa kidato cha Nne, Benedict
Herman alisema kuwa amejifunza uongozi na taaluma kwa kipindi alichosoma
shuleni hapo. “Nimejifunza mambo mbalimbali, nimejifunza uongozi, namna ya
kuzungumza na watu, stadi za maisha na taaluma imenisaidia kuongeza uelewa na
kupanua ubongo wangu. Kwa upande wa mtihani wa taifa wa kidato cha Nne,
maandalizi maandalizi ni mazuri na tuliweza kufanya mitihani mbalimbali tangu
kidato cha kwanza. Tumefanya mitihani ndani na nje ya shule kwa lengo la kujipa
uzoefu wa jinsi mitihani inavyotungwa. Matarajio yangu ni kuendelea na elimu ya
kidato cha Tano na Sita hadi chuo kikuu” alisema Herman.
Ikumbukwe kuwa Shule ya Sekondari Kisasa ilianza mwaka
2006 ikiwa na wanafunzi 20 na walimu watatu sasa ina wanafunzi 869 na walimu
55.
MWISHO
Comments
Post a Comment