Kata ya Makole yang’ara miaka minne ya Samia
Na. Emanuel Charles, MAKOLE
Diwani wa Kata
ya Makole, Omary Omary, aishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na
Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya maendeleo kwenye
sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, ujenzi wa barabara na ofisi ya
wafanyabiashara wadogo katika kata yake.
Akizungumza
katika ziara ya waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo
iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2020 hadi sasa katika Kata ya Makole, Diwani Omary
alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kuijali Kata ya Makole kuwaboreshea
miundombinu muhimu. “Kipekee nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miaka hii minne ambapo yupo madarakani, maboresho
ambayo ametufanyia hususani sisi wana Makole kwa kutuletea miundombinu sahihi
ni makubwa sana. Mheshimiwa Rais, ameboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule
ya jengo la ghorofa lenye madarasa nane na ofisi mbili za waalimu katika Shule
ya Msingi Makole. Katika sekta ya afya, Zahanati ya Makole sasa wananchi wote
wa kata yetu wanapata huduma ya afya nzuri na kwa usahihi, kuna hadi huduma ya
‘ultra sound’ hay ani mapinduzi makubwa. Tulitoa eneo kwa maelekezo kwaajili ya
ujenzi wa Ofisi ya Machinga Mkoa wa Dodoma na sasa imekamilika na inafanya kazi”
alisema Omary.
“Maboresho yote haya yana faida kubwa sana. Kwa mfano katika Shule ya Msingi Makole, utoro umepungua sana, watoto wanahudhuria masomo kwakuwa wanakaa kwa nafasi sasa. Kwa upande wa afya, huduma zimeboreka, vifaa tiba vipo na huduma ni nzuri” alisema Omar.
Nae, Katibu wa Machinga
Mkoa wa Dodoma, Victor Michael aliipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa
na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ameweza kutimiza ahadi aliyowaahidi kwa
kuwajengea ofisi ya wafanyabiashara wadowadogo (Machinga) ili kuweza kutatua
migogoro yao kama wafanyabiashara. “Rais wetu amekuwa akitusapoti sana sisi
wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma, tulimuomba kujengewa ofisi kila mkoa
kwaajili ya kushughulikia matatizo yetu na bila kusita alitoa fedha kiasi cha
milioni 10 na sasa tunafuraha kupata ofisi hii. Kwakweli, tunafuraha kubwa
sana, sasa tunafanya kazi zetu kwa uhuru na kwa kufuata utaratibu” alisema
Michael.
Katika hatua nyingine, Shule ya Sekondari Dodoma nayo imefanyiwa maboresho makubwa kwa kuongezewa vyumba vya madarasa, vitabu pamoja na kompyuta kwaajili ya kuongeza ufanisi na ujifunzaji kwa wanafunzi. Mwanafunzi wa kidato cha Sita, Joan Kilangi aliishukuru serikali kwa kuwaboreshea miundombinu ya kujisomea. “Sisi kama wanafunzi sasa hivi tunasoma vizuri kutokana na ongezeko la madarasa kwasababu hapo zamani tulikuwa tunakaa wengi katika chumba kimoja. Kwa sasa hatukai tena kwa kusongamana. Kwa namna ya kipekee, nipende kumshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutujengea madarasa haya, Mungu ambariki sana” alimalizia Kilangi.
MWISHO
Comments
Post a Comment