Mahakama zashauriwa kuyapa uzito mashauri ya kibiashara
Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MAHAKAMA
nchini zimeshauriwa kutoa umuhimu kwa mashauri ya kibiashara ili yaweze
kumalizika mapema na kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kuzalisha mali.
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria |
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria |
Kauli
hiyo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini
yaliyofanyika katika bustani ya Chinangali jijini Dodoma.
Rais,
Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema kuwa Mahakama nchini ziharakishe kusilimiza mashauri
ya kibiashara. “Tunapovutia mitaji na uwekezaji nchini na kufungua fursa za
kibiashara, tunatambua uwekezaji kuambatana na masuala ya kisheria na migogoro
ya kibiashara. Ni vema kwa Mahakama zetu kutoa umuhimu kwa mashauri ya aina
hiyo pia” alisema Dkt. Hassan.
Aidha,
alimpongeza Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuboresha utendaji katika Mahakama
nchini. “Mheshimiwa Jaji Mkuu nataka nikupongeze wewe na Mahakama kwamba hatua
nyingi mlizochukua zimekwenda kupunguza mambo mengi. Ucheleweshaji wa kesi
umepungua kwa kiasi fulani na kupunguza muda wa kesi kusikilizwa kwa muda mrefu
mahakamani” alisema.
Akiongelea
maendeleo ya kiuchumi na haki alisema kuwa vinauhusiano wa moja kwa moja. “Mheshimiwa
Jaji Mkuu, upo uhusiano mkubwa baina ya haki na maendeleo ya kiuchumi. Tunapoendelea
kuvutia mitaji nchini na kuendelea kuvutia fursa za wawekezaji, ni lazima
tuishi na kuzungumza ludha ya kibiashara na uwekezaji. Muwekezaji anathamini
sana muda kwa sababu muda ni mali. Na hapa namaanisha muwekezaji wa ndani na
yule wa nje. Ndiyo maana ni lazima mitazamo ya wadau wa Mahakama nchini
ijielekeze kwenye kupunguza muda unaotumika kwenye mashauri ili wananchi
watumie zaidi muda wao kwenye masuala ya uzalishaji.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma akikagua gwaride maalum
MWISHO
Comments
Post a Comment