Halmashauri ya Jiji la Dodoma Yatoa Mafunzo ya Malisho ya Mifugo
Na. Rehema Kiyumbi, DODOMA
Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji
la Dodoma Leonia Msuya ameendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya
kulisha na kutunza mifugo yao kwa maendeleo ya kiuchumi.
Aliyasema hayo wakati akiwa katika vipando vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maadhimisho ya kimataifa Nanenane. ’’Tumejiandaa kutoa elimu na kuonesha maonesho ya malisho ambayo ni chakula cha mifugo kwa sababu yamepanuka sana wananchi na wahamiaji wamekuwa wengi ambapo kusababisha malisho kupungua. Kwa mwaka huu tumeandaa vipando vitatu ambavyo ni malisho ya mikunde, nyasi na magugu (sumu) ambapo huchanganywa ili ng’ombe kupata virutubisho ambavyo ni protini, mafuta na wanga kama sisi binadamu,” alisema Msuya.
Alisema kuwa aina ya malisho ambayo ni
sumu huchangia kutoa elimu kwa wakulima na ni moja ya kutunza mazingira. ’’Sumu
ni aina ya malisho kama mihogo na nyanya tumefanya makusudi ili mkulima na
mfugaji kuweza kuyaondoa kwenye shamba lake. Pia, mkulima na mfugaji wakiandaa
mazingira vizuri ya kutengeneza malisho na kuyahifadhi ndani kutumika kwa mwaka
mzima au kuandaa shamba ili kuepusha mifugo kuzurura ovyo mitaani kutafuta
chakula,” alisema Msuya.
Aliendelea kutoa elimu kuwa watu wengi
hawafahamu majani ya mifugo hupandwa. “Watu wengi wamezoea majani ya mifugo
hayapandwi, ukweli ni kwamba majani hupandwa na mnyama huweza kula majani
makavu ili kumpatia virutubisho vya ziada kama madini kwa sababu baadhi ya
majani mabichi hukosa virutubisho. Pia, ni muhimu kwa sababu inamsaidia mfugaji
kujua idadi ya mifugo yake inakula malisho kiasi gani kwa siku na kulima majani
kiasi gani. Moja ya chakula kizuri kwa nguruwe na kuku ambapo wafugaji wengi
hawajui ni Alfa Alfa,” alieleza Msuya.
Alimaliza kwa kuwashauri wananchi hasa
wakulima na wafugaji wa vyakula vya mifugo kwa maendeleo ya jamii. “Tunawakaribisha
ili muweza kujifunza namna nzuri ya kuandaa mchanganyo wa malisho na kufahamu
majani tofauti tofauti yanayoingiliana kwa mifugo tofauti kama kuku, nguruwe, ng’ombe,
bata, sungura, pamoja na vyakula vingine vingi mifugo kupata virutubisho,” alimaliza
Msuya.
Mwisho
Imehaririwa na Samira Geregeza
Comments
Post a Comment