Na. Shahanazi Subeti, DODOMA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dodoma zilisaini mkataba wa TACTIC wenye thamani ya shilingi Bilioni 14.2 kwa lengo la kuboresha miundombinu, kuimarisha usimamizi wa uendelezaji miji na kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kukuza uchumi wa halmashauri ya jiji. Hafla hiyo ya Utiaji saini ilifanyika bustani ya Chinangali Park jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa soko kuu la majengo pamoja na ujenzi wa kituo cha daladala eneo la Mshikamano, Kizota na Nzuguni. Akielezea tukio hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa alisema, mikataba hii itakwenda kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa watanzania wanaoishi Dodoma na aliwaomba wakandarasi kutekeleza majukumu yao kwa wakati. "Tunapoboresha miundombinu hii itawafanya watanzania na wafanyabiashara, kuweza kusogeza biashara zao karibu, kuweza kutum...
Comments
Post a Comment